The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akutana na Mjumbe wa Mfalme wa Umoja wa Kiarabu

0

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 15, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Mfalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Shakhboot Al Nahyan Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Sheikh Al Nahyan amemshukuru Rais Samia kwa kuendeleza ushirikiano na nchi za Falme za Kiarabu na kumkabidhi barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Mfalme wa UAE, Sheikh Mohamed Bin Zayed Al Nahyan.

Katika mazungumzo hayo, Al Nahyan amesema UAE itaendeleza ushirikiano na uhusiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunga mkono usawa wa kijinsia na haki za wanawake na kuongeza kuwa umoja huo unaunga mkono jitihada za Rais Samia katika mapambano dhidi ya Covid 19 na kwamba upo tayari kuipatia Tanzania chanjo ya ugonjwa huo.

 

Leave A Reply