The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kukutana na Akina Mbowe, Zitto – Video

0

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema atakutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mwelekeo wa kuendesha shughuli za siasa zenye tija na maslahi kwa nchi.

 

 

Ameyasema hayo leo Alhamisi ya Aprili 22, 2021 wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi Machi 19, 2021.

 

 

Amesema amedhamiria kuendelea kulinda misingi ya demokrasia, uhuru wa watu na vyombo vya habari huku akibainisha kuwa uhuru na demokrasia ni msingi wa amani katika nchi na husaidia kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

 

 

“Katika kulinda uhuru wa demokrasia nakusudia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa Tanzania ili kwa pamoja tuweke mwelekeo wa kuendesha shughuli za siasa zenye tija na maslahi ya nchi yetu,” amesema Rais Samia.

Leave A Reply