The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Maalim Seif Alikuwa Daraja na Mwalimu – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Hayati Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa daraja na amani na mtu anayependa maridhiano ya kisiasa badala na malumbano na vurugu kama walivyo baadhi ya wanasiasa.

 

Rais Samia amesema hayo leo Ijumaa, Novemba 1, 2021 wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa maadhimisho ya maisha ya Maalim Seif ambaye alifariki dunia Februari 17, 2021.

 

“Nimesimama mikutano mingi kuongea na mingine ya kimataifa. Lakini sijaona ugumu kama naouona katika mkutano huu. Enzi za uhai wake, Maalim Seif alikuwa ni makutano ya watu, alikuwa ni kiongozi wa watu na alitokana na watu na watu walimshiba. Na huyo ndio Maalim Seif na watu kukutana leo kumkumbuka sio jambo la ajabu.

 

“Pamoja na kwamba Maalim Seif alifanya kazi ya ualimu hata kuitwa maalim, umaalim wake ni wa kipekee kutokana na kuwa hakuwa tu mwalimu wa wanafunzi bali pia alikuwa ni mwalimu wa watu. Maalim Seif alikuwa na uthibiti wa msimamo wake na alikuwa na utayari wa maridhiano hata pale unapotokea msigano. Na amefanya kazi hii ndani ya chama chake na katika vyama vingine.

 

“Tunaomfahamu Maalim Seif hata wakati akiwa CCM, enzi za chama kimoja alipokuwa na jambo alisimama na kuongea, na msimamo huo huo aliuendeleza hata alipohama na kuanzisha Chama cha Wananchi (CUF), alituheshimu na tulimuheshimu, hata alipotupinga hakuwa mwenye kutukana bali alitupinga kwa hoja.

 

“Utayari wake wa kuangalia maslahi mapana ya Taifa ndio ulifanya hata maridhiano yakapatikana na kufanya CCM na ACT Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hatuwezi kuizungumzia amani ya Zanzibar bila kumtaja Maalim Seif Sharif Hamad, Maalim Seif alikuwa ni daraja la amani na alitanguliza maslahi ya taifa mbele.

 

“Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa na mchango mkubwa wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi Zanzibar, alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kupigania kurejeshwa mfumo wa vyama vingi kuanzia mwaka 1989 hadi 1992.

 

“Siku za mwisho za uhai wake alihubiri ujumbe wa maridhiano na umoja wa kitaifa kokote alipopita, tutakumbuka alifunga safari yeye na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi kwenda kumuona Rais John Magufuli (Hayati ) ambapo alisema utulivu na amani ya nchi ndio jambo la muhimu.

 

“Maalim ingawa kuna wakati aliingiwa na kinyongo lakini alikuwa tayari kuzungumza kwa maslahi ya Taifa… alionyesha utayari wa kuzungumza. Ni mtindo mzuri kuenzi waasisi wetu walioleta mchango mkubwa kwa Taifa letu. Ni jambo zuri, na njia pekee ya kumuenzi Maalim Seif ni kuenzi umoja na mshikamano uliopo.

 

“Mara nyingi hasa katika nchi zetu zinazoendelea, wanasiasa wakitofautiana kinachofuata ni vurugu. Taswira hii hujitokeza hapa kwetu, lakini akiwepo mtu kama Maalim Seif vurugu hukatika na maridhiano yakaendelea. Mara nyingi hasa katika nchi zetu zinazoendelea, wanasiasa wakitofautiana kinachofuata ni vurugu. Taswira hii hujitokeza hapa kwetu, lakini akiwepo mtu kama Maalim Seif vurugu hukatika na maridhiano yakaendelea.

 

“Kama kuna somo Maalim Seif Sharif Hamad alilotuachia kwetu wanasiasa, ni kuwa tayari na kuwa na msimamo wa kutafuta maridhiano kwa wale ambao unakuwa na tofauti nao.

 

“Maalim Seif alikuwa na uthabiti wa msimamo wake na alikuwa na utayari wa maridhiano hata pale unapotokea msigano. Na amefanya kazi hii ndani ya chama chake na katika vyama vingine. Taasisi ya Maalim Seif Foundation ni yetu sote na tutaichangia, mkikwama katika masuala yoyote ya uendeshaji mtuone tuone tunasaidia vipi,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply