The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Sina Shaka na JWTZ – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu hassan amesema amani tuliyonayo inawapa wawekezaji uhakika wa mitaji yao na uhakika wa kufanya biashara na kupata faida, vilevile inaipa serikali wasaa wa kupanga shughuli za maendeleo kwa wananchi wake.

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu, Novemba 15, 2021 wakati akifungua Mkutano wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini na Makamanda wa Jeshi la Wananachi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar es Salaam.

 

“Nawashukuru (Vikosi vya Ulinzi na Usalama) kwa kuwezesha Taifa kuvuka salama baada ya msiba mzito wa aliyekuwa Amiri Jeshi wetu Mkuu na Rais Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Nawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya wakati ule, tunawashukuru sana.

 

“Sote tunafahamu kuwa amani na usalama ndio msingi wa maendeleo ya Taifa letu. Jeshi letu limepewa jukumu la kulinda na kusimamia ulinzi na usalama wa mipaka yetu na uhuru wa Nchi yetu. Jukumu hili kubwa na zito sana mmelifanya kwa takribani miaka 60 sasa.

 

“Naomba niwahakikishie kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuendelea kuliimarisha na kuliwezesha Jeshi letu kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiulinzi.

 

“Hatuna budi kuendelea kwa gharama yoyote ile kuitunza amani tunayojivunia ili iweze kuipandisha nchi yetu katika viwango vya juu vya maendeleo. Sina shaka na JWTZ katika kutimiza dhamana hii kubwa mliyoibeba.

 

“Kazi yenu mkishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imesimamia uwepo wa amani na utulivu nchini kwetu ambayo ni nyenzo muhimu sana kwa maendeleo yetu ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Nafahamu JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini mmevaa sifa zote za ubora,
umakini, uimara na umahiri katika kutimiza wajibu wenu.

 

“Katika kipindi kifupi ambacho umekuwa Rais takribani miezi saba umelifanyia Jeshi lako mambo makubwa ikiwemo kuidhinisha kupandisha vyeo kwa maaskari na maofisa waliostahili kupandishwa vyeo.” -Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply