The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Bunge Litakalokaa Septemba Kupitisha Bima ya Afya kwa Watu Wote

0
                   Rais Samia Suluhu Hassan Akiwa Kwenye Mkutano wa Jubilee ya Miaka 50 ya WAWATA

Rais Samia Suluhu Hassan katika adhimisho la jubilee ya miaka 50 ya WAWATA akiwa kama mgeni rasmi alisema serikali inakuja na mpango wa kutoa bima ya afya kwa watu wote ili kupunguza adha wanayopata wananchi katika kupata matibabu.

 

“Nataka niwape habari njema kwamba Bunge linakwenda kupitisha sheria ya Bima ya Afya kwa Watanzania wote…niwaombe sana ndugu zangu tutakapopitisha sheria hii…twendeni tukajiunge na mifuko ya Bima na ninataka niwahakikishie tunajua udhaifu uliopo kwenye mifuko yetu, tumechukua hatua tutakapoanza Bima ya Afya kwa wote, mfuko utakaosimama…utakuwa ni mfuko madhubuti” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Akisisitiza Watu Kujiunga na Mifuko ya Bima za Afya

Pia amesema baada ya kuanzisha mifuko hii ya bima watanzania inabidi wakajiunge kwa wingi ili kupata huduma Madhubuti wawapo kwenye vituo vya afya.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply