The House of Favourite Newspapers

Marekani Yaadhimisha Miaka 21 Tangu Shambulio Kubwa la Kigaidi ‘Septemba 11’

0
                                                    Shambulio la Septemba 11 New York Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris wamewaongoza Wamerekani kuadhimisha miaka 21 tangu kutokea kwa shambuliao la kigaidi katika majengo pacha ya World Trade Center na Pentagon.

 

Biden na Kamala walitembelea eneo hilo na kuiweka mashada ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka waliopoteza maisha kwenye sjhambulio hilo.

 

Familia za waathirika, maafisa wa polisi, wazima moto pamoja na wakuu wa mji wa New York, na  walikusanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Septemba 11, mahala ambako majengo mawili pacha ya World Trade Center yalibomolewa, na kusikiliza majina ya wale wote waliofariki yakisomwa.

                                       Mmoja ya waombolezaji katika eneo la Pentagoni Marekani

Watekaji nyara wa kundi la Al Qaeda waliteka ndege nne mnamo Septemba 11 mwaka 2001, mbili zikigonga na kuangusha majengo ya World Trade Center, ya tatu ikianguka kwenye jengo la Pentagon na ya nne kuanguka kwenye uwanja huko Pennsylvania.

 

Maadhimisho ya mwaka huu yanatokea mwaka mmoja baada ya  Rais Biden kuondoa wanajeshi nchini  Afghanistan na kumaliza vita  iliyodumu kwa miaika  20.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply