Rais Samia: Tuna ‘Crisis’ Ya Umeme, Tunafanya Ukarabati Wa Mashine – Video
Rais Samia Suluhu Hassan amempa miezi sita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ), Gissima Nyamo-Hanga kushughulikia tatizo la kukatika kwa umeme ili kuondoa kadhia hiyo kwa wananchi.
Nyamo-Hanga ameteuliwa kuchukua nafasi ya Maharage Chande ambaye ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.
Akizungumza kuhusu changamoto ya kukatika kwa Umeme katika Mikoa mbalimbali Nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi huzimwa ambapo husababisha upungufu wa umeme.