The House of Favourite Newspapers

Wadau na Wataalam wa Kimataifa Kuipa Temeke Mbinu za Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi

0
Manispaa ya Temeke inaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Mstahiki meya Abdallah Mtinika amekutana na wataalamu wa Taasisi ya Tomorrow ‘s Cities kutoka Uingereza.
Lengo la kikao hicho ni kuweka mikakati na kujenga uelewa wa namna jinsi ya kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yakiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua za El-nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mheshimiwa Mtinika amesema wanatarajia kufanya kikao kikubwa Septemba 28 mwaka huu ambapo wawakilishi wengine kutoka nchi mbalimbali watashiriki.
“Lengo kuu la mkutano huu ni kufanya Utafiti utakaosaidia wanatemeke kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa mafuriko na pia upangaji wa miji”.Alisema Meya Mtinika
Taasisi hiyo ya Tomorrow ‘s Cities itafanya Utafiti huo kwa kipindi cha miezi 6 ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es salaam anbapo itabaini changamoto zote zinazosababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo.
Kwa upande wake mtaalam kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es salaam Profesa Willbard Kombe amesema umuhimu wa Utafiti huu ni kwamba utasaidia kutambua ukubwa wa maafa na namna ya kuweza kukabiliana na maafa hayo.
Mwakilishi kutoka taasisi ya Tomorrow ‘s Cities  UCL,Bw.Mark Pelling amemshukuru Meya Mtinika kwa kuwaalika kufanya Utafiti huo katika wilaya ya Temeke na kusema kuwa Utafiti huu utaleta matokeo chanya na kuweza kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mkutano huu wa ufunguzi pia umewakutanisha maafisa Ardhi na mipango miji kutoka manispaa ya Temeke pamoja wataalamu wengine.
Leave A Reply