The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Tulifika Uchumi wa Kati Tukarudishwa “Tutarudi Uchumi wa Kati Kufikia 2025”

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kwamba ingawa Tanzania imeondolewa kwenye nchi zenye uchumi wa kati lakini kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa imefika au imekaribia kurudi uchumi wa kati.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Aprili 5, 2022 alipokuwa akihutubia katika hafla ya kufungua mkutano wa kitaifa wa haki, amani na maridhiano Tanzania ambao umefanyika Makao Makuu, Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma leo tarehe 05 Aprili, 2022.

“Tanzania tuliingia uchumi wa kati tukarudishwa, siyo kwa mipango ya mtu, ni mipango ya Mungu. Kwahiyo tupambane kurudi tulipokuwa. Na kwa ninavyoiongoza serikali, natarajia kufikia 2025 tutakuwa tumefika au tunakaribia kurudi uchumi wa kati” – Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Aidha katika hotuba yake, Rais Samia amewasisitiza viongozi wa vyama vya kisiasa kuhakikisha kwamba wanautumia mkutano huo vema na kumpelekea mapendekezo yenye tija kwa Tanzania na watu wake.

Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa, baadhi ya Mabalozi wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma kuhudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano, ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma leo tarehe 05 Aprili, 2022.

Rais Samia amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na hivyo wajadili mambo ambayo yanaendana na mazingira ya Kitanzania na kuongeza kwamba kazi ya vyama vingi ni kuona yanayofanywa na serikali na kutoa maoni kwa serikali.

Leave A Reply