The House of Favourite Newspapers

Rais wa China, Xi Jinping Achaguliwa Tena Kuongoza kwa Muhula wa Tatu

0

Rais wa China, Xi Jinping amechaguliwa tena leo Ijumaa Machi 10, 2023 kuwa Rais wa China ambapo ataiongoza Nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka mitano, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu utawala Mao Zedong.

Xi mwenye miaka 69 tayari alikuwa amepata nyongeza ya miaka mitano Oktoba 2022 kuwa mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha CCP na mwenyekiti wa tume ya kijeshi, nyadhifa mbili muhimu zaidi za madaraka nchini humo.

Bunge hilo pia limemchagua Zhao Leji kuwa Spika wake na Han Zheng kuwa Makamu mpya wa Rais.

Wakati huo huo Rais wa Urusi, Vladmir Putin amempongeza Rais wa China Xi Jinping kwa kuongezewa muhula mwingine wa tatu madarakani wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa Putin, anaamini kwamba watafanya kazi pamoja na watahakikisha kwamba wanaendeleza ushirikiano wa kimkakati kati ya Urusi na China katika nyanja mbalimbali.

HATIMAYE KAJALA AANIKA UKWELI WOTE PAULA KUOLEWA – ”PAULA NI MDOGO SANA”…

Leave A Reply