The House of Favourite Newspapers

Rais wa zamani wa CAR aliyetoroka ahukumiwa kifungo cha maisha jela

0

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliye uhamishoni, Francois Bozizé, amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 76, ambaye sasa anaongoza muungano wa waasi, alipatikana na hatia akiwa ugenini kwa mashtaka yakiwemo uasi na kudhoofisha usalama.

Ukitolewa siku ya Alhamisi, hukumu hiyo haikutoa maelezo yoyote juu ya muda au uhalifu unaohusika.Zaidi ya wengine 20, wakiwemo wana wawili wa Bw Bozizé, pia walipatikana na hatia bila kuwapo.

Bw Bozizé alinyakua mamlaka nchini CAR mwaka 2003.

Alipinduliwa muongo mmoja baadaye, na kusababisha vita vya mwisho vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeua maelfu ya watu.Sasa anaishi Guinea-Bissau.

#EXCLUSIVE: MZEE ALIYEIMBA ‘TANZANIA YETU’ ATAKUTOA MACHOZI-HAONI, ANAIMBA KWENYE BAA APATE KULA…

Leave A Reply