Rais Wa Zanzibar Dk Shein Atangaza Kuongeza Mishahara – Video
Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo Jumapili Januari 12, 2020 katika Uwanja wa Abeid Aman Karume.
Rais Shein amesema kutokana na makusanyo mazuri ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anaweza kuongeza mshahara kwa Watumishi kama jinsi marekebisho ya maslahi ya Wafanyakazi ya mishahara yalivyofanywa mwaka 2011, 2013,2015 na 2017.
Baadhi ya aliyoyasema kwenye hotuba yake:-
“Kila tunapoikumbuka siku hii muhimu tunapaswa tuwakumbuke viongozi wetu waliopigania taifa, wakiongozwa na jemedari wetu mzee Amani Abeid Karume. Tunamuomba Mungu awalaze mahali pema peponi waasisi wetu wa Mapinduzi”
“Serikali ya awamu ya saba ndani ya miaka 9 imeendelea kutekeleza mipango ya mageuzi ya kiuchumi kwa kuimarisha hali ya amani na kuongeza pato la uchumi mara sita zidi. Kutoka Trilioni 1.78 mwaka 2010 Trilioni 2.87 mwaka 2018”
“Kutokana na hali nzuri tunayokusanya, msishangae na mwaka huu nikikuongezeeni chochote kwa lengo la kuwapa motisha Wafanyakazi”.