The House of Favourite Newspapers

Rais Zelensky Awasihi Waukraine Kuendelea na Mashambulizi

0

Rais Volodymyr Zelensky amewaambia raia wa Ukraine “wamestahimili pigo” la uvamizi wa Urusi huku akiwataka raia kuendelea na mapigano.

 

Nje ya mji mkuu wa Kyiv, msafara mkubwa unaoenea zaidi ya maili 40 (64km) umesalia kukwama nje ya mji huo na maafisa wa ulinzi wa Ukraine wanasema wamekuwa wakilenga maeneo maalum ndani ya msafara huo pale wanapoweza.

 

“Mnahitaji kutoka nje na kutoa uovu huu nje ya miji yetu,” alisema.

Katika taarifa zingine:

Kumekuwa na mapigano makali kaskazini-magharibi mwa mji wa Kyiv katika mji uitwao Irpin, karibu na uwanja wa ndege wa kimkakati wa Hostomel na mkuu wa msafara wa Urusi.

 

Raia wamekuwa wakikimbia eneo hilo kwa miguu kujaribu kutafuta usalama
Maafisa wa Ukraine wanasema usitishwaji wa mapigano ulikubaliwa kuruhusu raia kuondoka mji wa bandari wa Mariupol ulioko kusini mwa nchi hiyo na ulidumu kwa dakika kadhaa siku ya Jumamosi kabla ya mashambulizi kuanza tena.

 

Urusi inachukulia eneo la kusini kuwa muhimu kwa mafanikio ya uvamizi wake na watu katika bandari ya Odesa wanaogopa kushambuliwa na Urusi kutoka baharini.

 

Miji ya Kharkiv na Sumy katika eneo la mashariki pia imekuwa ikishambuliwa upya kwa mabomu.
Urusi ilisema imesonga mbele kwa kilomita 7 (maili nne) katika mkoa wa Donbas, ikichukua miji na vijiji kadhaa.

Leave A Reply