The House of Favourite Newspapers

RAIS ZUMA KUJICHIMBIA STUDIO KUREKODI ALBAMU

RAIS Mstaafu wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anakusudia kuingia studio hivi karibuni, kurekodi albam ambayo itakuwa na nyimbo za mapambano.
Uongozi wa mji wa Durban, mji mkuu wa jimbo lake la KwaZulu-Natal, umetangaza kuwa utafadhili gharama za kurekodi albamu hiyo.

Mkuu wa kitengo cha burudani na utamaduni wa mji huo, Thembinkosi Ngcobo amesema  kuwa wazo hilo lilifikiriwa miaka mitatu iliyopita.

“Tulikuwa tunatafuta wasanii wa nyimbo za aiana hii, ilikuwa ngumu , tulijaribu kutafuta hata video fupi fupi, lakini hatukupata kitu katika jumba la makumbusho, hapo ndipo kama Idara tukamkumbuka Zuma kwenye suala la kuimba.
”Hivi karibuni tulikuwa na Mazungumzo na Zuma, tulienda nyumbani kwake, tukajadili, alianza kuongelea mengine lakini kabla hatujaondoka, alisema amefurahi kuwa sehemu ya ‘ptoject’ hiyo, hivyo tutaangalia namna ya yeye kufanya mazoezi na kwaya hivi karibuni,” ameeleza Ngcobo.

Comments are closed.