The House of Favourite Newspapers

Rapa Diddy Apata Msiba Mzito, Mastaa Marekani Wampa Pole!

Rapa Sean Diddy Combs amepata msiba wa aliyekuwa mama wa watoto wake watatu, ‘Kim Porter’ ambaye ameaga dunia jana Alhamisi, Novemba 15, 2018 akiwa na umri wa miaka 47.

 

Mtu wa karibu familia amethibitisha kifo hicho kupitia Mtandao wa Page Six; “Kwa masikitiko nathibitisha kuwa tumepata msiba wa Kim Porte, wanafamilia wapo kwenye majonzi makubwa,” alisema mwanafamilia huyo.

 

Kim Porte alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Homa ya Mapafu (Pneumonia) kwa muda wa wiki moja lakini haijajulikana kama ugonjwa huo ndiyo umesababisha kifo chake.

 

Mahusiano ya Porte na Diddy yalianza mwaka 1994 na kuachana 2007 wakiwa na watoto watatu, mapacha wa kike Jessie James na D’lila na mtoto wao mwingine Christian.

 

Baadhi ya Mastaa wa Marekani wamempa pole Diddy kupitia akaunti zao za Twitter wakiwemo, 50 Cent, Missy Eliot, Rick Ross, Kehlan, Juicy J na wengine.

Nimekuwekea Tweets hapa chini.

EXCLUSIVE: AY Afunguka “Sio Diamond tu, Hata mimi Nilishafungiwa “

Comments are closed.