The House of Favourite Newspapers

Rasmi Azam FC Wampiga Chini C.E.O Saad Kawemba

0

Azam FC yenye makazi yake eneo la Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, imemalizana na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa klabu hiyo Saad Kawemba, na sasa hatakua tena sehemu ya  klabu hiyo.

Taarifa za uhakika kutoka kwa moja ya viongozi wa klabu hiyo, zimesema uongozi wa Azam FC umefikia makubaliano mtendaji huyo jana Juni Mosi na kumpa mkono wa kwaheri, hawatakua nae tena katika klabu yao.

Habari za Saad kuondoka Azam zilianza kuvuma kwenye mitandao takribani wiki moja, na kesho uongozi huo unatarajia kutangaza rasmi juu ya uamuzi huo.

Kabla ya mkurugenzi mtendaji wa Azam, Kawemba alikua Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu  (TFF).

Leave A Reply