The House of Favourite Newspapers

Rasmi Klabu ya Manchester United Yawekwa Sokoni, Glazers Wasalimu Amri

0
Mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakiandamana kupinga uwekezaji wa Familia ya Glazer ndani ya klabu hiyo

HATIMAYE klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza imewekwa sokoni ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 17 ya umiliki chini ya familia ya kitajiri ya Glazer kutoka nchini Marekani.

 

Thamani ya Manchester United sokoni inakadiriwa kuuzwa kwa Paundi Bilioni 5 na taarifa za awali zimebainisha kuwa kama klabu hiyo itauzwa basi itauzwa kwa muwekezaji kutoka Marekani kama ilivyo kwa familia ya Glazer.

 

Kwa kipindi kirefu mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakiandamana kushinikiza wamiliki hao kuondoka ndani ya viunga vya Old Trafford, huku nyota Cristiano Ronaldo ambaye naye amesitishiwa mkataba wake na klabu hiyo akianika wazi udhaifu wa wamiliki hao katika kuendeleza mafanikio ya Manchester United ambayo ni moja kati ya klabu kubwa nchini Uingereza na Dunia kwa ujumla.

Rasmi familia ya Glazer ambao ni wamiliki wa klabu hiyo wameiweka sokoni Manchester United

Manchester United inakadiriwa kuwa na wafuasi zaidi ya Bilioni 1,2 duniani kote hivyo kuifanya kuwa moja ya klabu zenye thamani kubwa kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa mashabiki na wafuasi.

 

Taarifa kutoka Manchester United imesema:

“Mbinu za kimkakati zinafanyika na mchakato huu utaangalia namna mbalimbali ikiwemo uwekezaji mpya, Kuuzwa kwa klabu au mchakato mwingine unaohusisha Kampuni.

 

Tutapitia michakato yote kuhakikisha tunawasaidia mashabiki pamoja na Klabu kwa ujumla kuhakikisha inaendelea kukua na kupata fursa nyingine kwa sasa na siku za baadaye.”

Leave A Reply