The House of Favourite Newspapers

Rasmi Mugalu Atua Simba Akitokea Power Dynamo ya Zambia

0

CRIS Mugalu mshambuliaji aliyekuwa anakipiga ndani ya Power Dynamo ya Zambia, leo Agosti 16 ametambulishwa ndani ya Simba.

Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili na anaungana na washambuliaji wawili tegemeo ndani ya Simba ambao ni John Bocco na Meddie Kagere.

Bocco na Kagere wamekuwa na pacha nzuri msimu wa 219/20 ambapo wote wapo Kwenye kikosi bora cha msimu.

Kwa pamoja wamehusika Kwenye mabao 31 kati ya 78 yaliyofungwa na Simba ambayo imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kagere alifunga mabao 22 na Bocco alifunga mabao 9 hivyo nguvu ya ushambuliaji inaongezeka kwa Mabingwa hao wa Ligi mara tatu mfululizo.

Leave A Reply