The House of Favourite Newspapers

Wahitimu Wa Ubunifu Wote Wapata Ajira Kwenye Mahafali

0
Mmoja wa wahitimu akimuonesha baadhi ya kazi walizojifunza, mgeni rasmi, Jahari Sadiq (kushoto) kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo hicho, Anna Peter.

Wahitimu wa chuo cha ubunifu wa mavazi, mitindo na teknolojia cha Institute of Fashion and Technology (IFT) jana walionesha umahiri wa kazi zao mbele ya wageni waalikwa walihudhuria kwenye mahafali yao yaliyofanyika chuoni hapo, Mwenge TRA jijini Dar.

Mhitimu akipita mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) na vazi alilojishonea mwenyewe.

Katika mahafali hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa mbunifu mkongwe wa mavazi nchini, Johari Sadiq wahitimu hao walionesha kazi mbalimbali walizojifunza chuoni hapo.

Huyu naye akipita na gauni alilojishonea baada ya kupata mafunzo.

Miongoni mwa vipaji walivyoonesha wahitimu hao ni jinsi ya kuchora nguo kabla ya kuishona na jinsi ya kutengeneza kitambaa kuwa nguo ya kuvaa wakitumia pini.

Wakionesha kipaji cha kuichora nguo kabla ya kuishona.

Wahitimu hao wakiwa wamevaa nguo walizojishonea wenyewe walionesha fasheni shoo mbele ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo.

Bango la chuo hicho.

Akizungumza kwenye mahafali hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Anna Collection ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa chuo hicho, Anna Peter alisema hayo ni mahafali ya kwanza ya chuo hicho.

Hawa walionesha ubunifu kwa kukibana kitambaa kwa pini na kutokea gauni kama linaloonekana katikati yao.

Anna amesema walichokionesha wahitimu hao ni steji tu ya awali ya kozi yao ambapo kuna kozi zingine mbili wanatakiwa kuzisomea chuoni hapo ili waweze kukomaa zaidi na kuingia kwenye soko la ajira ya kiushindani.

Mkurugenzi Mtendaji wa chuo hicho, Anna Peter ‘Anna Collection’ akiongea mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) kushoto ni mkuu wa chuo hicho.

Katika neema iliyowadondokea wahitimu hao waliokuwa 14 kutokana na vipaji walivyoonesha wote walipata ajira kutoka kampuni moja ya ubunifu wa mitindo hapa nchini kabla ya kuendelea na kozi zingine walizotakiwa kuendelea nazo.

Mmoja wa wahitimu akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi, Johari Sadiq.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL  

Leave A Reply