The House of Favourite Newspapers

RAY kwa Mwanaye Humwambii kitu!

Vincent Kigosi ‘Ray’

LEGENDARI wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefunguka kuwa tangu amekuwa baba, ratiba yake ya kurudi nyumbani imebadilika tofauti na miaka ya nyuma alipokuwa anarudi muda wowote anaotaka. Akizungumza na Amani hivi karibuni, Ray alisema tangu awe mzazi, amejikuta akiwawahi kurudi sana nyumbani na kuacha mambo mengi ya ujana maana anaona ni wakati sasa wa kulea na kumfundisha mwanaye malezi bora.

“Daah sasa hivi mimi kabla ya saa mbili lazima niwe nimerudi nyumbani labda itokee bahati mbaya sana. Narudi bwana mwanangu mwenyewe asiponiona tu ni tatizo,” alisema Ray ambaye amezaa mtoto huyo wa kiume na mwigizaji, Chuchu Hans.

Stori: Erick Evarist

Comments are closed.