RAY: NISINGEFANANA NA JADEN, NINGEPATA TABU SANA!

Vincent Kigosi ‘Ray’

LEGENDARI wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefunguka kuwa asingefanana na mwanaye aitwaye Jaden, angetukanwa sana.Akizungumza na Amani juzikati, Ray alisema, anamshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kufanana naye kwani vinginevyo walimwengu wangemsumbua kwa maneno ya kejeli.

“Walimwengu bwana wanaongea sana. Ingetokea mtoto labda kafuata kwa mama kila kitu halafu kwangu hamna kitu, yangeibuka ya kuibuka hadi ungeshangaa, nashukuru sana Jaden amenifichia maneno kwa kufanana na mimi,” alisema Ray.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Loading...

Toa comment