The House of Favourite Newspapers

Ray Vanny anogesha ubingwa wa Liverpool Dar

Baadhi ya mashabiki wakifurahia ushinfdi wa Liverpool dhidi ya Totenham kwenye kombe la mabingwa ulaya.

 

 

 

WAKATI mashabiki wa Liverpool wakishangilia kwa msisimko baada ya timu yao kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya sita, wapenzi wa kandanda zaidi ya 1,600 walijikusanya katika ukumbi wa Next Door Arena, jijini Dar es Salaam kushuhudia tukio hilo.

 

Huku mechi hiyo ikiendelea, msanii wa Bongo Fleva, Ray Vanny aliyeletwa ukumbini hapo kwa udhamini wa Heineken, aliwaburudisha mashabiki waliokusanyika katika eneo hilo.

Liverpool walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa kombe hili baada ya kuichapa Tottenham Hotspurs 2-0 jijini Madrid huku mabao ya washindi yakifungwa na Mohamed Salah kwa njia ya penalti huku Divock Origi akitikisa nyavu mwishoni mwa kipindi cha pili.

Ikiwa mmoja wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo maarufu na inayotizamwa na mamilioni ya watu kote duniani, kampuni ya Heineken ilifanikisha mashabiki hao kushuhudia mechi hiyo ya kukata na shoka.

“Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni moja kati ya ligi zinazohusisha wachezaji wakubwa. Timu zote bora barani Ulaya zinashiriki ligi hii. Kwa upande mwingine, bia ya Heineken ni bia inayojulikana na kutumiwa na watu wengi kote duniani  na kwa hiyo kuna uhusiano kati ya Heineken na ligi ya mabingwa. Mwaka huu, wateja wetu siyo tu wamefurahia kutazama ligi bali pia kushiriki fursa zinazokuja na ligi,” alisema Meneja wa Heineken Tanzania, Lungisa Adams.

 

Meneja huyo aliongeza kuwa kinywaji hicho kinatengeneza msisimko katika ligi hiyo yenye utajiri mkubwa kwa vilabu Barani Ulaya.

 

Kwa mujibu wa Lugisa, Heineken imetoa haki za kipekee kwa mashabiki kuweza kushiriki katika kutizama fainali katika mazingira tulivu na ya aina yake kwenye ukumbi wa NEXT Door Arena, jijini Dar es Salaam.

 

 

 Fainali hii pia ilitizamwa katika sehemu tofauti tofauti 8 mbali mbali nchini.

Lungisa aliongeza kuwa, wateja wa Heineken waliweza kushiriki pamoja na kubadilishana taarifa za matukio wakati wakitazama fainali kupitia kibwagizo  #ShareUnmissableMoments.

 

Alisema ikiwa kama bia yenye jina kubwa, siku zote imekuwa ikidhamini na kuwekeza kwenye michezo ambayo inayowagusa wateja wake na kuwaleta pamoja katika masoko yanayochipukia kama Tanzania.

Comments are closed.