The House of Favourite Newspapers

Rayvanny na Paula Wadaiwa Kulala Hoteli Moja

0

LICHA ya kwamba wenyewe hawajathibitisha moja kwa moja, madai mazito yametua kwenye RISASI MCHANGANYIKO kuwa, staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na mtoto wa mwigizaji wamelala hoteli moja, karibu upate ubuyu!Ubuyu unaeleza kuwa, wawili hao walinaswa hivi karibuni wakizama hoteli moja iliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo kutoka kwenye hoteli hiyo (jina linahifadhiwa ) kimeliambia RISASI kuwa, kilimuona Rayvanny na Paula wakiwa wanaingia kwenye hoteli hiyo mida ya jioni jioni. “Njoeni haraka nipo hapa nje nimemuona Rayvanny na Paula wanaingia hapa hotelini, Global nyinyi nawaami,” alisema mpashaji huyo wa kuaminika.

HABARI KAMILI

Baada ya kupokea kwa simu hiyo mwandishi wetu alifunga safari moja kwa moja hadi eneo la tukio ili kujua ukweli juu ya habari hiyo na kufika hadi mapokezi na mahojiano na mtu wa mapokezi yalikuwa hivi.

 

Mwandishi: Habari yako mzima wewe?

Mapokezi:Salama kabisa, karibu nikusaidie… Mwandishi: Samahani nilikuwa nauliza chumba (anazuga). Mapokezi: Karibu sana, jisikie huru.

 

Mwandishi: (anaulizia kizushi) lakini pia kama nimeona gari la Rayvanny hapo nje yupo hapa nini maana natamanigi kumuona live?

Mapokezi: Jamani wewe mbona kunitafuta maneno mimi jamani si unajua maadili ya kazi yetu sisi haturuhusiwi kuzungumza tunayoyaona hapa…

 

Mwandishi: Najua ila nilitaka unisaidie maana nampenda sana Rayvanny…

 

Mapokezi: (anakuwa mkali kidogo) Kwani umekuja kuulizia chumba au umekuja kufatilia mambo ya watu? Hapa Rayvanny hayupo…

MWANDISHI AMPOTEZEA

Mwanahabari wetu baada ya kuona mbinu ya kwanza imeshindikana, aliamua kurudi kwa chanzo cha awali kilicho jirani na hoteli hiyo na kukipa kazi ya kuendelea kufuatilia zaidi.“Hamna neno kama mtanipoza kwa kuwa mimi nipo hapa jirani, nitafatilia halafu nitawaambia,” kilisema chanzo hicho.

 

RAYVANNY ATUPIA PICHA

Kesho yake, Rayvanny alitupia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilimuonesha akiwa na Paula wamegeukia dirishani ikiwa imepigwa kwa nyuma.“Kuna mtu kaniambia wametupia picha lakini wamejipiga kwa nyuma angalia kwenye ukurasa wa Rayvanny,” kilisema chanzo hicho.

 

RISASI liliingia kwenye ukurasa wa Rayvanny na kujionea picha hiyo ambayo ilizua gumzo kwa watu kuhoji kulikoni Kajala amruhusu mwanaye huyo aanze kujiachia na Rayvanny wakati bado alikuwa na mpango wa kuendelea na shule.Hata hivyo, baadhi ya mashabiki kwenye ukurasa huo wa Instagram, walimtetea binti huyo kuwa aachwe kwani ameshafika umri wa miaka 18.

 

WALALA USIKU KUCHA…

Kesho yake, majira ya mchana, mpashaji huyo alisema kuwa tangu waingie muda wa jioni, walitoka saa sita mchana. “Yani tangu waingie jioni huwezi amini ndiyo wametoka saa sita ya mchana ila wamekuwa makini sana hata wakati wanatoka nimeshindwa hata kuwapiga picha,” kilisema chanzo hicho.

 

WENYEWE WANASEMAJE?

Baada ya kuweza kukusanya data za kutosha kutoka ndani ya hoteli hiyo, mwanahabari wetu aliwatafuta wawili hao, ili waweze kuzungumzia juu ya madai hayo.Kwa bahati mbaya, simu ya Paula haikuweza kupatikana lakini Rayvanny alipokea na kuomba atafutwe baadaye yupo kwenye makelele.“Nipo kwenye kelele nikikaa sehemu nzuri nitakupigia,” alisema Rayvanny.

 

TUJIKUMBUSHE

Miezi kadhaa iliyopita, kuliibuka msala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya Rayvanny kuvujisha vipande vya video vilivyomuonesha akibusiana na Paula.

 

Kajala ambaye wakati huo alikuwa kwenye penzi motomoto na staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ aliandika bonge la waraka mtandaoni na kumshutumu mwanamitindo Hamisa Mobeto kuhussika kumtorosha mwanaye, kumlewesha na kupiga video hizo.

 

Msala huo ulitinga kwenye kituo cha Polisi Oysterbay lakini hata hivyo taarifa zinaeleza walimalizana kimyakimya na Kajala na Paula wakaenda zao Dubai kula bata.

 

Baada ya kurudi, Paula na Rayvanny wanaonekana kuendeleza vitendo vya kimahaba kupitia mitandao ya kijamii na maisha yakiendelea na Kajala akionekana kupoteze

STORI MWANDISHI WETU, RISASI

Leave A Reply