The House of Favourite Newspapers

Rayvanny: Paula Mke Wangu, Amkana Fahyma

0

WAKATI baadhi ya mashabiki wake ‘wakiwa rada’ kusikilizia kama zile video alizojirekodi mwanamama Fahyma akiwa kitandani kwa Rayvanny ni mpya au ni za zamani, jamaa huyo ameibu mapya.


Baada ya kuona kama ishu hiyo
inaaminika, Rayvanny ameona isiwe kesi ameamua kuhamisha mada kwa kurudisha mpira kwa mpenzi wake wa sasa, Paula Kajala.

 


Ikumbukwe kwamba hapa
katikati, baada ya Paula kwenda masomoni nchini Uturuki, kumeibuka mambo mengi ikidaiwa kwamba, Rayvanny amerudiana na Fahyma ambaye ni mama wa mtoto wake wa kiume aitwaye Jaydany.

Pia ni kama vile Rayvanny alikuwa amepunguza kasi ya kumpsiti na kumimbia Paula kama ilivyokuwa awali.Lakini ghafla, wikiendi iliyopita, Rayvanny alivunja ukimya ambapo aliposti picha yake akiwa amekumbatiana na Paula kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kisha akaandika: “Miss you my wife!”


Akimaanisha amemmisi Paula ambaye
ni mke wake!Maswali yamekuwa ni mengi mno kwani baadhi ya mashabiki wanajiuliza Rayvanny alishamuoa Paula hadi amuite mke wake?

 

Hata hivyo, wakati Rayvanny akimuita Paula wife, mrembo huyo yeye amekuwa akimuita Rayvanny daddy!

Leave A Reply