The House of Favourite Newspapers

RC Charamila Kushiriki Mbio za Km Tano na 10 Zilizoandaliwa na TCAA

0
Mwenyekiti wa Maandalizi ya Maadhimisho ya Kusherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mellenia Kasese (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam kuhusiana na mbio za mashindano ya ridhaa “Fun Run” zilizoandaliwa na mamlaka hiyo.
MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam  Albert Charamila anatarajiwa kushiriki kushiriki mbio za km tano  na  km 10 zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) zitakazofanyika Oktoba 29, 2023 katika viwanja vya Mlimani City.
Mwenyekiti wa maandalizi ya Maadhimisho hayo Mellenia Kasese ameyabainisha hayo Jijini Dar es salaam mapema leo Oktoba 26, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini kuhusiana na mbio hizo amesema mbio hizo ni sehemu ya muendelezo wa matukio ya kusherehekea miaka 20 ya taasisi hiyo ambayo tangu ilipoanzishwa.
Amesema lengo mbio hizo  ni  kutunisha mfuko wa upandaji miti katika katika jamii hasa katika maeneo ambayo ni kame .
“Mbio za mashindano ya ridhaa “Fun Run” zitakazoanzia Mlimani City na kuishia hapo zikiwa na lengo la kuhamasisha upandaji na utunzaji wa miti katika mikoa yenye ukame,”amesema
Amesema mbio hizo zitakuwa za km tano na kumi, maandalizi yameshakamilika vifaa vyote vimeshafika na hadi sasa tiketi zote 400 ambazo zilitengwa kuuza kwa ajili ua washiriki zimeshaisha siku tatu nyuma, ambapo tiketi moja ilikuwa Sh 20,000.
Pia, amesema TCAA inatarajia kukutana na wadau wa sekta ya anga ili kujadili mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzisha kwa mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Maandalizi ya Maadhimisho ya Kusherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mellenia Kasese (katikati) pamoja na Katibu wa Chama Cha Riadhaa  Mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela wakionesha vifaa ambavyo vitatumika katika mbio hizo zitakazofanyika kwenye viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam
“Mjadala huu unatafanyika Oktoba 30,2023 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) uliopo Dar es Salaam, mgeni rasmi anatarijiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassimu Majaliwa,” amesema
Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Riadhaa  Mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela ambao ndiyo wasimamizi wa mbio hizo amesema   tangu awali wamekuwa wakishirikiana na TCAA katika  maandalizi ya mbio hizo wamekuwa walishirikiana vyema katika maandalizi kutokana na chama hicho ndio limekuwa kikiusika katika mbio zote.
Mwela amesema wamejiridhisha na wamehakikisha njia zitakazotumika, zimepimwa na ni salama, ambapo wanasubiri Jumapili kwa ajili yakuhitimisha tukio hilo.
Aidha, alitoa wito kwa wadau wengine wanaofanya mbio za hisani kushirikiana na Chama hicho ili kuweza kuepukana na chagamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.
“Kumekuwa na changamoto kwa watu wengine kutohusisha chama cha riadha wanapoandaa mbio ni hatari sana ukipata jambo utakuwa hauna pakupeleka kama hivi wamefanya jambo la kuhimu na kuweza kujua nini chakufanya,”amesema Mwela.
Leave A Reply