The House of Favourite Newspapers

RC HAPI AWAJIBU WAANDISHI: “WEWE NANI UNANIPA SIKU 7” – VIDEO

RC wa Iringa Ally Hapi akizunguzmia sakata la Chama cha Wanahabari wa Mkoa wa Iringa kumpa siku 7 aombe radhi baada ya kuwataka nao kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Jumatatu ya Mei 27 wakati akiuzungumza na watendaji, Hapi alisema… “Wafanyabiashara ni wengi kuna wapiga debe, wauza nyanya, mchicha, wachoma mahindi na hata waandishi wa habari na wapiga picha wote wanatakiwa kuwa na vitambulisho ili kuchangia kodi kutokana na kazi wanazofanya.”

 

Jumanne Mei 28, 2019, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Frank Leornald alisema kauli ya Hapi inadhalilisha taaluma ya habari. Alisema waandishi wa habari mkoani humo wamefanya majadiliano na kuazimia mambo sita watakayoyawasilisha katika ofisi ya mkuu huyo wa Mkoa, na kutaka majibu ya haraka.

Akizungumzia kutakiwa kuomba radhi, Hapi amesema yeye kama Mkuu wa Mkoa anamwakilisha Rais Magufuli, hivyo hakuna mtu wa kumpa siku saba Rais kwa mumwamuru afamye jambo flani.

RC HAPI AWAJIBU WAANDISHI – “WEWE NANI UNAMPA MKUU WA MKOA SIKU 7”

Comments are closed.