The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Akabidhi Majina 97 kwa Kamishna Mkuu wa Kupambana na Dawa za Kulevya

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akionesha kabrasha lenye majina 97 ya watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, kulia ni Bw. Rogers William Sianga ambaye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya. Makonda akionesha kabrasha lenye majina ya watuhumiwa.

Makonda akikabidhi majina hayo kwa Kamishna Rogers William.

Wakikabidhiana.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga akizungumza .

Makonda akizungumza na waandishi wa habari na wadau.

Awamu ya tatu ya oparesheni maalum ya kutokomeza madawa ya kulevya nchini, imeendelea kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuitisha mkutano na waandishi wa habari pamoja na viongozi wengine wengi wa mkoa, ambapo kwa pamoja wameendelea kusisitiza kwamba vita hiyo ya madawa ya kulevya ni endelevu na wataendelea kupambana kuhakikisha madawa ya kulevya yanaisha Dar es Salaam na wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa, Makonda amemkabidhi orodha ya watu 97 wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya ambapo amemkmabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga. Juu ni picha za makabidhiano hayo, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa mwalimu Julius Nyerere, Posta jijini hapa.

PICHA ZOTE NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISERS

Comments are closed.