The House of Favourite Newspapers

RC Mjini Magharibi Azindua Kampeni ya Ujenzi wa Madarasa

0
RC Ayoub Mahmoud.

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Ayoub Mahmoud, amewaomba watu wote kujitokeza kutoa misaada ya hali na mali ili kuwezesha kuendeleza na kukamilisha ujenzi wa madarasa katika mkoa wake.

 

Mahmoud aliyasema hayo katika uzinduzi wa mpango wa ‘Mimi na Wewe’ unaolenga kuondoa upungufu wa madarasa katika mkoa huo katika shule mbalimbali. Shughuli hiyo ambayo imezinduliwa leo na kufanyika katika eneo la Kijito Upele unalenga kujenga madarasa 54, ambapo leo umeanza kwa ujenzi wa madarasa manne ulioshirikisha wananchi wengi wa eneo hilo.

 

Shughuli hiyo ni kampeni kubwa iliyozinduliwa Mei 21, mwaka huu na Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha tatizo la madarasa katika shule mbalimbali linatatuliwa kwa wananchi kujitolea kwa hali na mali.

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO

Leave A Reply