RC Mtanda Ahamishiwa Mwanza, Kanali Mtambi Ateuliwa RC wa Mara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuhamisha Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akichukua nafasi ya CPA Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha,Rais Dkt.Samia amemteua pia Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Mtanda ambapo kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.