Rais Samia Atengua uteuzi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Joyce Ndalichako
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Deogratius Ndejembi aliyekuwa Naibu Waziri wa Tamisemi kushika nafasi iliyoachwa wazi na Ndalichako.