The House of Favourite Newspapers

Redcross Mkoa wa Kilimanjaro Wamwagiwa Sifa kwa huduma Zao Kili Marathon 2022

0
Mratibu wa Redcross mkoa wa Kilimanjaro, Mohammed Omary Kisima akiwa kwenye harakati za kutoa huduma kwa wakimbiaji na wengine waliofurika Uwanja wa Chuo cha Ushirika kushuhudia Kili Marathon 2022.

 

 

JANA Jumapili ilikuwa ni siku ya kipekee Moshi mkoani Kilimanjaro kutokana na tamasha kubwa la mbio za Kilimanjaro Marathon kilometa 42, 21 pamoja na kutembea kilometa 5 huku Shirika la Msalaba Mwekundu Redcross likimwagiwa sifa kwa jinsi lilivyoendesha zoezi la utoaji wa huduma ya kwanza.

Redcross wakimsaidia mmoja wa wakimbiaji aliyezidiwa wakati akimaliza mbio za kilometa 21.

 

 

 

Katika mbio hizo zilizoanzia Chuo Cha Ushirika Moshi, takribani wakimbiaji na watembeaji zaidi ya 12,000 kutoka zaidi ya mataifa 55 yalishiriki katika mbio hizi jambo ambalo lilileta taswira mpya katika mkoa wa Kilimanjaro.

Huyu naye akipelekwa kupatiwa huduma ya kwanza.

 

 

Shukrani za dhati zilitoka kwa serikali ya awamu ya sita ya Mama Samia Suluhu Hasani ambazo ziliwakilishwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Kasim.

 

Miongoni mwa sifa zilizomwagwa katika kufanikisha mbio hizo pamoja na waratibu wa mbio hizo Executive Solution, wadhamini wakuu wa mbio hizo Kilimanjaro Premium Lager  wengine ni Redcross mkoa wa Kilimanjaro kwa kujipanga vema kuwahudumia kwa haraka na kitaalam wale wote waliokumbana na changamoto zilizohitaji huduma ya kwanza.

Huduma za uokoaji zikiendelea.

 

 

Katika mbio hizo, Red Cross ilihusika kama mdau wa afya katika idara ya utoaji wa huduma ya kwanza kwa wakimbiaji na watazamaji walioshiriki Kilimanjaro Marathon 2022.

Mkiambiaji akipelekwa kupata huduma ya kwanza.

 

 

Pamoja na pongezi hizo kwa Redcross changamoto kwa upande wao zilikuwa nyingi kubwa ilikuwa ni hali ya hewa iliyosababisha watu wengi kuanguka kutokana na hali ya joto kali iliyojitokeza kipindi hiki.                                                                                                                                                                                                  HABARI/PICHA ZOTE NA ISAACK MAKOI /GPL 

Leave A Reply