The House of Favourite Newspapers

Rekodi za Jembe Jipya Yanga Zinatisha

0

REKODI za winga mpya wa Yanga, Chico Ushindi zinatisha jambo ambalo linaonesha ni kweli timuhiyo imepata jembe la maana ambalo litakuja kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inazidi kuwa kiwembe.


Yanga tayari imekamilisha
usajili wa mkopo wa winga huyo ambaye alikuwa anakipiga katika Klabu ya
TP Mazembe ya nchini DR
Congo.


Katika mkataba huo, kuna
kipengele cha nyota huyo anayetumia miguu yote kusakata kabumbu kujiunga
na Yanga moja kwa moja
kama wataridhika na uwezo wake au kumuuza kisha fedha wagawane na TP Mazembe.

 


Ushindi ambaye kwa sasa
ana umri wa miaka 25, anamudu vema kucheza nafasi zote za mbele akiwa anacheza winga ya kulia na kushoto, lakini pia anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati namba 9 na wa pili namba 10.


Raia huyo wa DR Congo
ambaye alijiunga na TP Mazembe msimu wa 2017/18, amefanikiwa kuichezea timu hiyo michezo 72 katika misimu minne na kuhusika kwenye mabao 47, akifunga 30 na kutoa asisti 17.

 


Pia amefanikiwa
kuitumikia timu ya taifa ya DR Congo katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza
ligi ya ndani (CHAN) iliyofanyika mwaka huu nchini Cameroon ambapo
alifunga mabao mawili na
kutoa asisti moja.

STORI; MARCO MZUMBE, DAR

Leave A Reply