The House of Favourite Newspapers

Rekodi Za Raundi Ya Pili Zaibeba Simba SC

0

JOTO kubwa la jiji kwa sasa ni mchezo wa Yanga na Simba ambao unatarajiwa kuchezwa Machi 8, kwenye Uwanja wa Taifa ambao utakuwa ni wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

 

Kwenye mchezo wa kwanza ambapo Simba alikuwa mwenyeji alishindwa kuondoka na ushindi kwa kulazimisha sare ya mabao 2-2.

Kuanzia msimu wa 2009/10 mpaka 2018/19 zimekutana mara 10, Simba imeshinda mechi sita huku Yanga ikishinda mbili na sare mbili.

Katika mzunguko wa pili mabao 17 yamefungwa huku Simba ikifunga mabao 11 na Yanga ikifunga 6, idadi kubwa ya mabao yalipatikana msimu wa 2011/12 ambapo Simba ilishinda mabao 5-0 mzunguko wa pili.

 

Mechi ambazo Simba ilishinda mzunguko wa pili: 2009/2010 Simba 4-3 Yanga, 2011- 12 Simba 5-0 Yanga, 2014/15 Simba 1-0 Yanga.

 

2016/17 Simba 2-1 Yanga, 2017/18 Simba 1-0 Yanga, 2018/19 Yanga 0-1 Simba.

Zilizotoshana nguvu msimu wa 2010/2011 Simba 1-1 Yanga, 2013/14 Simba 1-1 Yanga.

 

Yanga ilishinda mechi mbili ambazo ilikuwa ni msimu wa 2012/13 Yanga 2-0 Simba, 2015/16 Yanga 2-0 Simba.

Hivyo, kuelekea keshokutwa Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya sare ya 2-2 Januari 4, 2020. Wafungaji kwa Simba walikuwa ni Meddie Kagere na Deo Kanda wakati Yanga wafungaji walikuwa ni Mapinduzi Balama na Mohamed Issa.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

Leave A Reply