The House of Favourite Newspapers

Ridhiwani alivyomvaa Dk Kigwangalla

MBUNGE wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amemvaa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala akimwambia kwamba bado hajafanya kazi yake vilivyo katika kutangaza vivutio vya utalii nchini.

Ridhiwani aliyasema hayo jana katika uzinduzi wa redio ya kutangaza utalii ya Hakuna Matata.

Alisema hivi karibuni alimuona Dk Kigwangalla akipiga picha katika moja ya mbuga za wanyama kama njia ya kuhamasisha kutembelea vivutio vya utalii.

 

“Nilipoiona ile picha, nilimkosoa kwa kweli na kumwambia bado hajaweka nguvu kubwa kwenye ushawishi, ingekuwa vizuri kama angetumia wasanii ambao wana watu wengi wanaowafuatilia kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete.

Kuhusu ujio wa redio hiyo, Ridhiwani alisema ni jambo zuri ukizingatia kuwa ni ya mtandaoni ambako dunia imehamia huko.

 

Awali akieleza lengo la kuifungua, mkurugenzi wa redio hiyo, Beatrice Ndungu alisema moja ya sababu ni kutangaza utalii na pia kuzalisha ajira kwa vijana.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali akiwemo Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune, Mzee Chilo na Monalisa.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Comments are closed.