The House of Favourite Newspapers

Rio Aionya Man United Kwa Tripper

0

BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, ameionya timu hiyo juu ya ishu ya kutaka kumsajili beki wa Atletico Madrid, Kieran Tripper.

 

Rio amesema Man United hawahitaji kumsajili beki huyo zaidi wanatakiwa kuangalia mchezaji mwingine.

Trippier mwenye miaka 30, aliondoka Tottenham mwaka 2019 na kujiunga na Atletico ambayo msimu wa 2020/21 ametwaa ubingwa wa La Liga.

“Sifikirii kama wanahitaji kumnunua mchezaji wa aina yake ambaye anahitaji kucheza kila siku, wanatakiwa kumleta mchezaji ambaye atakuwa anasaidiana na mchezaji aliyepo sasa.

 

Walitumia pauni 50m ambazo ni fedha nyingi kumsajili Wan-Bissaka, halafu leo hii aje kukaa nje, hiyo sio sahihi.“Niwe muwazi, Trippier kwangu sio chaguo sahihi japo ana ubora.

 

Hawezi kuwa chaguo langu kutua pale na kucheza kama beki wa kulia,” alisema Rio.

Leave A Reply