The House of Favourite Newspapers

Rekodi: Afariki Akiacha Gumzo Wake 39, Watoto 94

0

ZIONA Chana mwanamume anayeaminika kuwa na familia kubwa ya wake 39 na watoto 94 amefariki dunia Juni 14, 2021, huku akicha gumzo kubwa.

 

Chana alifariki dunia akiwa na miaka 76, katika jimbo la Mizoram kaskazini mashariki mwa India, huku akiacha wajukuu 33 na vitukuu kadhaa. Gumzo kuhusu mwanamume huyo inatakana na jinsi alivyoweza kuhudumia familia hiyo kwa mahitaji ya kila siku ikiwamo chakula, malazi na mavazi pamoja na huduma nyingine muhimu.

 

Hata hivyo, alipohojiwa katika miaka ya hivi karibuni, Chana alieleza kuwa aliamini kuwa ni mtu aliyebarikiwa kuwa na familia hiyo.

Ziona Chana ni nani?

Chana alikuwa na familia yenye jumla ya watu 167 walioishi katika nyumba moja yenye ghorofa nne na wastani wa vyumba 100 katika kijiji cha Baktawng Tlangnuam.

 

Chana alifariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu, Chana pia alikuwa akiishi na wakwe 14 (wanawake walioolewa na watoto wake wa kiume) na wajukuu 33.

 

Mwanaume huyo aliyekuwa na wake 39 mpaka anafariki dunia alidai kuoa mkewe wa kwanza akiwa na miaka 17 mwaka 1959 na kuna kipindi alioa wake 10 ndani ya mwaka mmoja.

 

Familia hiyo, iliyokuwa kivutio cha watalii pia iliishi katika kijiji cha Mizoram na ilipewa jina la ukoo wa “Chana” ambalo lilitungwa na baba wa Ziona mwaka 1942.

 

Katika jumba hilo kulikuwa na bweni moja kwa ajili ya wake zake wote lililopakana na chumba chake maalumu ambapo yeye alipenda kulala na wake zake saba au nane kwa wakati mmoja.

 

Wake zake walikuwa wakifanya zamu kulala naye, kila mmoja alikuwa akijua ratiba yake. Licha ya ukubwa wa familia hiyo alikaririwa akiiambia Reuters kwamba alitamani kuiongeza zaidi, kwani anaamini alikuwa ni mtu aliyebarikiwa Alipohojiwa miaka ya hivi karibuni, Chana alisema kwenye mlo wa jioni walikuwa wakitumia kuku 30, kilo 60 za viazi na kilo 100 za mchele kwa mlo mmoja.

Na vyakula hivyo vilipikwa kwa pamoja katika jiko moja.

Leave A Reply