The House of Favourite Newspapers

RIPOTI KUTOKA INDIA ..PASCAL CASSIAN TAA YA KIJANI

KAMA wewe ni shabiki wa muimbaji wa muziki wa Injili aliyewahi kuwa mshindi katika Shindano la Bongo Star Search ‘BSS 2009’ Pascal Cassian, taarifa mpya ikufikie kwamba, taa ya kijani imemuwakia ikimaanisha kwamba, hali yake inaendelea vizuri baada ya hivi karibuni kutua India kwa ajili ya matibabu. 

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu Pascal alisema alipofika na kufanyiwa vipimo, hatua ya kwanza ilikuwa kufanyiwa oparesheni ya kibofu cha mkojo na kwa sasa yuko kwenye hali inayotoa matumaini.

 

“Kwa kweli naweza kusema kuwa Mungu mkubwa kwa sababu sikutarajia kufikia hali hii, nashukuru nimeshafanyiwa oparesheni ya kibofu cha mkojo, nilikutwa na mawe.

“Madaktari wamefanikisha zoezi hili lakini pia kuna dawa ambazo nimepewa, naendelea kuzitumia nafikiri nitakuwa sawa maana hali niliyokuja nayo siyo niliyo nayo sasa hivi. “Lakini niendelee kuwashukuru Watanzania kwa maombi ambayo wanayafanya kwangu, nawaomba wasichoke kuniombea ili niweze kurudi salama na kama Mungu akipenda Ijumaa ninaweza kurudi Tanzania,” alisema Pascal.

 

Siku za hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dare s Salaam, Paul Makonda alifanikisha mpango wa kumpeleka msanii huyo nchini India kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali ya gari na kusababisha aumie paja na kupasuka kibofu cha mkojo. Gazeti hili linamuombea msanii huyo apone haraka ili arejee kwenye shughuli za kulijenga taifa.

Stori: NEEMA ADRIAN, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.