The House of Favourite Newspapers

Ripoti ya CAG Yaondoka na Bosi wa Utalii

0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha, Ndumbaro amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya CAG.

 

Waziri Dr.Ndumbaro ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

 

“Nafasi ya Mdachi itakaimiwa na Betrita James ambaye ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi TANAPA, hatuwezi kumchunguza Mtu akiwa kakalia kiti hichohicho,” amesema Ndumbaro.

Leave A Reply