RIYAMA AWAPONDA WANAOTOA SIRI ZA WAUME ZAO!

STAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ally amewaponda wanawake wanaopenda kutoa siri za waume zao au wanaume wanaoachana nao na kusema huo ni ulimbukeni wa kupitiliza.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Riyama alisema tabia hiyo imekuwa ikimkera sana na yeye kwenye maisha yake hawezi kuthubutu kufanya hivyo.

“Mimi mwanaume hata nikiachana naye siwezi kwenda kumtangaza madhaifu yake kwa watu wengine, kufanya hivyo nitakuwa namdhalilisha na kujidhalilisha mimi mwenyewe “Hivi mwanaume ambaye umetoka naye unaanzaje kumtangaza madhaifu yake halafu wewe ukaikwepa aibu?” alihoji Riyama ambaye wakati anaongea na mwandishi wa habari hii mumewe aitwaye Mystereo alikuwa pembeni yake.

 

STORI: RICHARD BUKOS

Toa comment