The House of Favourite Newspapers

JPM Kutatua Kitendawili cha Ujenzi Kituo cha Daladala Uyole – Video

RAIS  John  Magufuli amewataka wananchi wa Uyole mkoani Mbeya kuwa wavumilivu wakati akitafuta njia ya kutatua ombi lao la kupewa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi madogo (daladala) na Soko la Uyole.

 

 

Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu, Aprili 29, 2019, wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo mamlaka yake imeliona kwa muda mrefu kuwa linafaa kwa ujenzi wa kituo hicho ni lililo Uyole, lakini likiwa linamilikiwa na kampuni moja ya Kichina iliyopewa kwa ajili ya kuendeleza kilimo.

Hayo yalifuatia mkuu wa mkoa huo kumweleza kuwa kama hilo likishindikana, wanaomba kuchukua sehemu ya eneo la Shule ya Msingi Uyole na sehemu ya chuo cha Uyole ili kufanikisha ujenzi huo, lakini rais amesema wampe muda azungumze na watalaamu wa ardhi ili waone namna ya kuwapa eneo kwa ajili ya mradi huo.

 

“Nimezisikia hizo changamoto naomba mniachie,” alisema rais akiwahakikishia ameyapokea malalamiko yao.

 

MSIKIE MAGUFULI AKIZUNGUMZA

Comments are closed.