The House of Favourite Newspapers

Robin van Persie Aukubali Usajili wa Cavani Man U

0

STRAIKAwa zamani wa Manchester United, Robin van Persie, amesema angalau safari hii klabu hiyo imeweza kusikiliza mawazo yao kwa kusajili mtambo wa mabao, Edinson Cavani.

 

Man United ilifanikiwa kumsajili Cavani siku ya mwisho ya usajili kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na PSG.

Mbali na Cavani, wengine waliosajiliwa na Man United msimu huu ni Donny van de Beek, Alex Telles, Amad Diallo na Facundo Pellistri.

 

Van Persie alisema: “Walau Man United safari hii wamesikia kwa kumsajili Cavani. Ni usajili mzuri, kutokana na uzoefu wake atakuwa msaada kwenye timu na kuwasidia wenzake.”

Leave A Reply