The House of Favourite Newspapers

Roger Federer Yupo Karantini Katika Mjengo Wa 19B

0

KWA Tanzania mchezo wa tenisi umekuwa hauna umaarufu mkubwa na kuna ambao wanaona ni mchezo fulani wa kishua, lakini wapo ambao wamekuwa wakiucheza na ni watu wa kipato cha chini.

 

Mataifa yaliyoendelea ni mchezo wenye mashabiki wengi, Roger Federer ni mmoja wa nguli wa mchezo huo, ambapo kwa sasa yupo katika mapumziko baada ya michezo kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

 

Mkali huyo wa tenisi ni mmoja wa wanamichezo matajiri ambaye anamiliki mijengo kadhaa pia, lakini gumzo ni ule wa wenye thamani ya pauni 6.5m (Sh bilioni 19).

Nyumba hiyo ya kitajiri inaweza kukufanya ubadili mawazo yako kuhusu mchezo huo kwa kuwa mjengo huo wenye ghorofa tatu akiwa pia anaishi na wazazi wake, Robert na Lynette, unaweza kukufanya ubadili mawazo yako kuhusu mchezo huo.

 

Nyumba hiyo ipo pembezoni mwa Ziwa Zurich, alianza kuijenga kuanzia mwanzo na mwisho kuhamia mwaka 2014.

 

Ndani ya mjengo huo kuna bwawa la kuogelea na kuna mgawanyiko kwa sehemu mbili za familia kuishi.Hadi sasa Federer amefanikiwa kuingiza pauni 450m (Sh trilioni 1.2) kutokana na mchezo wa tenisi tangu alipoanza kucheza akiwa ameshinda mataji mbalimbali yakiwemo nane ya Wimbledon.

 

 

Mjengo huo ni wa kifahari kweli, ndani kuna gym kubwa yenye vifaa mbalimbali, sehemu ya kuegesha magari kwa chini, lakini kwa jumla ukubwa wa eneo lote analomiliki ni ekari 1.5.

 

 

Uzuri ni kuwa katika mjengo huo ameugawa mara mbili, Federer anaishi na familia yake katika mjengo huo, akiwa na mkewe, Mirka pamoja na watoto wao wanne, Myla, Charlene, Lenny na Leo.

Leave A Reply