The House of Favourite Newspapers

Roma Adaiwa Kuwatenga Mastaa Wenzake

Staa wa Bongo, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’.

HITMAKER wa Ngoma ya Zimbabwe, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ anadaiwa kuwatenga mastaa wenzake ambao wamepitia naye katika muziki.

 

Kwa mujibu chanzo, Roma amekuwa na tabia ya kuanzisha urafiki na wasanii wenzake kwa kipindi kifupi kisha wanazinguana, alianza ushkaji na rapa mwenzake, Jose Mtambo wakazinguana, akaja Dayna Nyange naye wakatosana.

 

“Kuna msanii anaitwa Kala Jeremiah, walikuwa marafiki kweli hadi kwenye harusi ya Roma alitoa sapoti kubwa naye wakazinguana na sasa hivi Stamina, ile projekti yao ya Rostam imekufa na sababu ni kwamba wamezinguana,” kilisema chanzo.

 

Bongo Flevani ilimsaka Roma kujibu madai haya na alipopatikana alianza kwa kucheka sana;

“Hizo habari umetoa wapi? Sikiliza nikwambie, hakuna kitu kama hicho, tangu nimeanza muziki huu sijawahi kuzinguana na mwana yeyote kwa hiyo hizo habari hazina ukweli wowote,” alisema Roma.

Comments are closed.