The House of Favourite Newspapers

Roma Amjibu Harmonize Kisa Nigeria

0

BAADA ya msanii wa Bongo Fleva,  kusema kuwa kuna wasanii wa Bongo wanajiona wakubwa, lakini nyimbo zao hazipigwi nchini Nigeria, rapa mkali Bongo amejibu juu ya ishu hiyo.

 

Akiwa nchini Nigeria, msanii Harmonize alifunguka mambo yanayoonesha pamoja na juhudi kubwa ambazo wasanii wa muziki Afrika Mashariki wanazifanya kuhakikisha kuwa muziki wa ukanda huu unapenya kila kona ya Afrika na dunia, lakini bado safari ni ndefu.

 

Harmonize, akiwa nchini humo alifanya mizunguko katika sehemu mbalimbali za starehe ikiwemo kwenye klabu ndipo akagundua kuwa muziki wa Afrika Mashariki, bado haujakua mkubwa kama vile wasanii wa Afrika Mashariki wanavyodai.

Kwa mujibu wa Harmonize, alisikia nyimbo mbili tu zenye sauti za wasanii wa Bongo zikipigwa huko ambazo ni wimbo wake wa Anajikosha na Sere wa Olakira wa Nigeria akiwa amemshirikisha Zuchu na Attitude ambao alidai kuwa unapigwa kwa heshima ya staa mkongwe wa muziki wa dansi Awilo Longomba tu ambaye alimshikisha.

Hata hivyo, baada ya ukimya f’lani, Roma naye ameibuka na mtazamo wake juu ya sakata hilo ambapo anasema; “Uzalendo ni somo pana Sana!! Leo ukicheza Kiduku unaonekana mshamba na umepitwa na wakati, lakini wenzetu South (Afrijka) mimi toka mdogo nawaona wanacheza Kwaito na mpaka leo wanaicheza na hatuoni kama ni washamba.

“Hata ile syle ya mapanga shaaa kiumeni ilikuwa ni ya kikwetuKwetu kabisa, tulipaswa tuishi nayo wote mpaka leo.

“Kipi sahihi hapa; vyetu hatuvithamini, ndiyo maana na wao hawavithamini na hawaviigi?

“Vyetu haviwavutii ndiyo maana hawaoni umuhimu wa kuviiga?

“Hatuna uzalendo, tuna shobo?”

Leave A Reply