The House of Favourite Newspapers

Mtangazaji Dida Afunga Ndoa Serena Dar

0

Taarifa zinaeleza kwamba jana Juni 10, 2021 mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’ alifunga ndoa katika Hoteli ya Serena jijini Dar lakini hata hivyo mumewe, mpaka sasa hajaonekana.

 

Jitihada za wadaku wa Kipindi cha Hot Pot kumpata mwamba huyo zimegonga mwamba mpaka jana usiku wa manane. Hata hivyo, jitihada zaidi zinaendelea na atakapopatikana, tutamwanika hapa.

Video mbalimbali  zilizovuja zinamuonesha Dida akiwa amevalia shela la harusi akiwa kwenye hoteli hiyo ya Serena peke yake bila ya mumewe.

 

Pia ipo video ambayo inamuonesha mkono wake na wa huyo jamaa na mkono wa Dida.

Hii ni ndoa ya nne kwa mtangazaji huyo. Dida aliwahi kuolewa na Juma Mchopanga ‘Mchops’, Gervas Mbwiga ‘G’ kabla ya kuolewa na mtangazaji mwenzake, Ezden Jumanne Ntambi na wote hao ameshatemana nao.

STORI NA ERICK EVARIST

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply