The House of Favourite Newspapers

Ronaldo Apelekwa Karantini

0

WAKATI wachezaji wa Juventus wakianza mazoezi baada ya kuelezwa Serie A ipo njiani kurudi tena, staa wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo amepelekwa karantini.

Ronaldo ambaye alikuwa kwao Ureno kwa mapumziko baada ya ligi hiyo kusimama kutokana na uwepo wa corona, mapema wiki hii alirejea Italia na kupelekwa karantini kwa siku 14.

Mapema wiki hii, Juventus walianza mazoezi chini ya uangalizi maalum ili kujiepusha na maambukizi ya corona.

Baadhi ya mastaa walioo-nekana wakianza mazoezi ni Giorgio Chiellini, Aaron Ramsey na Leonardo Bonu-cci.

TURIN, ITALIA

Leave A Reply