The House of Favourite Newspapers

Ronaldo Atwaa Ballon d’Or kwa Mara ya 5, Awabwaga Messi, Neymar

Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo yake.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo huku akiwabwaga mpinzani wake wa karibu Lionel Messi.

Ronaldo ameitwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano na kuwa sawa na Messi ambae pia ametwaa kwa mara tano.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi, na Timu ya Taifa ya Argentina amekuwa wa pili huku mchezaji mahiri wa PSG ya nchini Ufaransa, Timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr, akitwaa katika nafasi ya tatu.

Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012.

Ballon d’Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote.

LIVE: Birthday ya WOLPER! Alivyoingia Ukumbini kwa Mbwembwe!

Comments are closed.