Ronaldo, Salah Wawania Tuzo Uefa

Cristiano Ronaldo.

MASTAA watatu kwenye soka Mohamed Salah, Cristiano Ronaldo na Luka Modric ndiyo wamepitishwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya, Uefa.

 

Jambo ambalo limeonekana kuwa la ajabu ni kukosekana kwa staa wa Barcelona, Lionel Messi ambaye amedumu kwenye tuzo hiyo kwa miaka zaidi ya kumi.

Salah ameingia kwenye vita hiyo baada ya msimu uliopita kufanya kazi kubwa na kuiongoza Liverpool kumaliza kwenye nafasi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Staa huyo wa Misri alifanikiwa kufunga mabao 44, kwenye msimu huo na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu England.

 

Kwa upande wa Ronaldo yeye ameingia hapa baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Huu ulikuwa ubingwa wa tano kwa staa huyo raia wa Ureno, lakini pia akiwa alimaliza mfungaji bora wa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

 

Lakini kwa upande wa Modric, yeye ameingia kwenye vita hii baada ya kufani-kiwa kut-waa Ligi ya Mabi-ngwa akiwa na Real, lakini kigezo kikubwa ni kiwango cha juu alichoonyesha kwenye fainali za Kombe la Du-nia amb-apo aliiwe-zesha nchi yake ya Croatia kufika fainali.

 

Mbali na kufika hapo, pia Modric alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo.

 

Mshindi wa tuzo hii anatarajiwa kutangazwa Agosti 30 mwaka huu, wakati wa upangwaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Zurich Uswisi.


Loading...

Toa comment