The House of Favourite Newspapers

Rose Ndauka: Siendekezi starehe

MWANAMAMA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Rose Ndauka amesema yeye siyo mtu wa kuendekeza starehe kwenye maisha yake, hivyo kitu pekee alichoruhusu kimtawale ni kazi tu na si vinginevyo.

Akistorisha na Za Motomoto News, Rose alisema anajua kutumia fedha lakini siyo kwa kuendekeza starehe, kitu pekee anachoruhusu kimtawale katika maisha yake ni kazi maana ndiyo anaamini inamfanya kila mtu amuone bora.

“Starehe nafanya lakini siyo kupita kiwango, kuna muda nikifanya sana kazi na kupata fedha nyingi ndiyo naenda kujiburudisha sehemu, lakini sifanyi starehe kama ndiyo sehemu ya maisha yangu. Kazi ndiyo nimezipa kipaumbele sana kwa sababu zinaniingizia pesa na kunipa heshima mjini,” alisema Rose.

STORI  MEMORISE RICHARD

Comments are closed.