The House of Favourite Newspapers

Ruangwa Jimbo Cup Yaibua 7 Kwenda Namungo-20

0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ameshuhudia mechi ya fainali ya mashindano kuwania kombe la Jimbo la Ruangwa ambapo Nkeng’ende FC iliichapa Mkangano FC 5-1.

 

Katika mechi hiyo iliyochezwa jana (Septemba 4, 20201) kwenye uwanja Shule ya Awali Msingi ya Wonder Kids, Mheshimiwa Majaliwa alisoma majina saba ya wachezaji ambao watajiunga na kambi ya timu ya vijana ya chini ya miaka 20 ya Namungo FC.

 

Waziri Mkuu alisema kuwa lengo la masindano hayo lilikuwa ni kuuibua vipaji kwa vijana ambao baadae wataichezea Namungo FC ya wilani Ruangwa.

 

Mashindano ya kuwania kombe la Jimbo la Ruangwa yalishirikisha 32 kutoka Kata za Jimbo hilo ambapo mshindi wa kwanza alipata kombe, kitita cha sh. milioni mbili, seti moja ya jezi na mpira.

 

Mshindi wa pili alijipatia shilingi Milioni Moja na nusu, seti moja ya jezi na mpira na mshindi wa tatu shilingi milioni moja, seti moja ya jezi na mpira.

 

Wakizungumza baada ya kuwa wametajwa kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji wa Namungo chini ya miaka 20, vijana hao wamepongeza maandalizi ya michuano hiyo nakuahidi kutumia fursa waliyoipata katika kuinua kiwango cha soka kwenye timu hiyo na Jimbo la Ruangwa.

 

Naye, Kapteni wa Timu ya Nkeng’ende FC alisema siri ya wao kuchukua ubingwa ni maandalizi waliyoyafanya katika kipindi chote cha michuano pamoja na nguvu ya mashabiki ambao walijitokeza muda wote wa michuano.

Leave A Reply